pmbet

Diamond,Alikiba na Harmonize rasmi kutifuana ulingoni mmoja kutwaa tuzo.

Joyce Shedrack

August 29, 2024
Share :

Kamati ya uandaaji wa Tuzo za Muziki nchini (TMA)  imetangaza rasmi majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume wa mwaka.

Wasanii waliotangazwa kuwania kipengele hicho ni Marioo kupitia ngoma ya 'Shisha’, Diamond ‘Shu’, Harmonize ‘Single Again’, AliKiba ‘Sumu’ na mwisho ni Jay Melody na wimbo wa ‘Nitasema’.

Vigezo vya kushinda tuzo hizo kwa wasanii washindani waliotangazwa ni kupigiwa kura na mashabiki na tayari waandaji wa tuzo hizo wametangaza kufungua dirisha la kupiga kura kuanzia siku ya jumannne ya wiki ijayo.

 

Wasanii watakaowania vipengele vingine katika tuzo hizo watatangazwa hivi karibuni na waandaji wa tuzo hizo (TMA).

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet