Dini chanzo cha sisi kuchelewa kufunga ndoa - Chuchu Hans
Eric Buyanza
June 6, 2025
Share :
Kutoka kiwanda cha Bongo Movie, muigizaji maarufu Chuchu Hans, amesema licha ya kuishi pamoja na mzazi mwenzake Vicent Kigosi ‘Ray’ lakini kikwazo kikubwa cha wao kushindwa kufunga ndoa ni dini.
Chuchu amesema utofauti wa dini yeye akiwa muislam na mwenzake mkristo ni miongoni mwa mambo yanayoleta mvutano na hivyo hajui ni lini hasa watafunga ndoa.
“Nimekuwa kwenye mahusiano zaidi ya miaka kumi. Siri ya kudumu ni kujitambua na kujenga msingi imara wa maisha. Lakini ukiona mtu hashiki mkono wako kwenda mbele, ni lazima ujitathmini,” amesema.
TSN