Djokovic agoma kustaafu akiwataja Ronaldo na James
Sisti Herman
October 17, 2025
Share :
Staa wa mchezo wa tenis duniani, Novak Djokovic amesema wazi kwamba hana mpango wa kustaafu kucheza tenisi katika siku za usoni.
Akiwa kwenye Joy Forum 2025, alizungumzia uvumi wa kustaafu moja kwa moja, akisema, "Ninajua kuna watu wanataka nistaafu, lakini hilo halitafanyika," akiongeza, "Haifanyiki. Samahani kuwakatisha tamaa. Siyo sasa."
Uamuzi wa Djokovic umechangiwa na hamu ya kucheza muda mrefu katika mchezo huo, akiwataja wanariadha kama LeBron James, Cristiano Ronaldo, na Tom Brady kama motisha ambao wamecheza vyema hadi miaka ya 30 na 40.
Alionyesha msukumo mkubwa wa kuona "ni umbali gani naweza kufika" na kuwa sehemu ya mustakabali unaoendelea wa mchezo huo. Anaamini kuwa tenisi inafanyika mabadiliko makubwa na anataka kubaki hai kitaaluma ili kushuhudia na kuchangia mabadiliko haya.
Licha ya kufika nusu fainali ya michuano yote minne ya Grand Slam mwaka wa 2025 na kukabiliwa na masuala ya utimamu wa mwili, Mserbia huyo mwenye umri wa miaka 38, ambaye kwa sasa ameorodheshwa nambari tano duniani, bado ameazimia kuendelea kushindana katika kiwango cha juu zaidi.