pmbet

DOGE yamshtaki mke wa Biden kwa kutomjali Mumuwe

Sisti Herman

May 21, 2025
Share :

Mke wa Rais aliyepita wa Marekani Joe Biden, Jill Biden ametakiwa kufikishwa mahakamani, akituhumiwa kutojali afya ya mumewe mzee.

 



Pendekezo la kumpeleka Jill Biden kortini lilipendekezwa na Leo Terrell, ambaye anakuwa afisa wa kutekeleza sheria katika idara ya uangalizi ya serikali inayosimamiwa na Elon Musk (DOGE).

Leo Terrell alisema kunapaswa kuwa na uchunguzi unaolenga kufahamu iwapo Jill Biden hakumshinikiza mumewe kuwania kiti cha urais wa Marekani, akijua wazi kuwa alikuwa na saratani.

Usiku wa Jumapili, Mei 18, 2025, ilitangazwa kuwa Joe Biden alikuwa amegunduliwa na saratani ya kibofu.

Joe Biden, ambaye aliongoza Marekani kwa muhula mmoja, hakuweza kuwania muhula wa pili kwa sababu ya masuala ya afya ambayo yalizuia chama chake cha Democratic kumteua.

Nafasi yake ilichukuliwa na Kamala Harris wakati huo kuwania kiti cha urais wa Marekani, lakini akaishia kushindwa na Donald Trump.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet