Drake afata nyayo za Diamond Platnumz azindua manukato yake.
Joyce Shedrack
April 30, 2025
Share :
Rapa maarufu mwenye asili ya Kanada Aubrey Drake Graham maarufu Drake ametambulisha manukato ‘parfume’ yake anayouza kwa gharama ya dola $148 sawa na Shilingi laki 398,000/= za Kitanzania.

Drake anaingia kwenye kundi la Wasanii wa muziki wanaojihusisha na biashara mbalimbali huku wakiwa na bidha zao wenyewe sokoni.
kwa hapa Tanzania mwanamuziki aliyejitahidi kufanya kitu kama hicho ni Diamond Platnumz ambaye yeye aliyeyapa jina manukato yake CHIBU perfume ambalo ni jina alilopenda kujiita lakini Drake ameipa bidhaa yake hiyo mpya jina la ‘Summer Mink .