pmbet

Gabo apita na mchezaji wa ligi kuu kwenye Baraluko.

Joyce Shedrack

May 13, 2025
Share :

Muigizaji namba moja nchini Tanzania, Salim Ahmed maaarufu kama Gabo Zigamba leo amefanya uzinduzi rasmi wa tamthilia mpya fupi inayojulikana kwa jina la BARALUKO mbele ya vyombo vya habari na wadau mbalimbali wa sanaa ambayo amesema amemshirikisha ndani mchezaji wa mpira anaekipiga ligi kuu Tanzania Bara.

 

Hii ni hatua muhimu sana kwa Gabo kama msanii kinara wa maigizo nchini Tanzania Pamoja na Afrika Mashariki na kati kwa kutambua kiu ya mashabiki zake Pamoja na wadau wasanii ambao wamekaa mkao wa kula tangu walipoburudika na kuelimika katika tamthiliya ya Mawio.

 

Ikumbukwe Gabo ni msanii wa maigizo raia wa Tanzania mwenye mamilioni ya wafuasi kutoka maeneo mbalimbali Duniani hivyo basi kuwaletea mashabiki zake hao tamthilia hii ya Baraluko kumezingatia hitaji la wadau wa sanaa la kupata burudani Pamoja na elimu katika tamthilia hii ambayo imechezwa nchini Tanzania ikiangazia mila na tamaduni za Mtanzania.

 

Tamthilia hii ya Braluko imedhamiria kuonesha maisha ya Mtanzania yaliyobeba uzuri na ugumu wa mahusiano ya kifamilia sanjari na hilo pia imelenga kutoa elimu kwa jamii sambamba kuibua mijadala Chanya kwenye jamii yenye lengo la kujenga na kutengeneza hoja zenye mashiko katika jamii yetu.

 

Tamthilia hii yenye mvuto wa kipekee inawahusisha waigizaji wakubwa akiwemo Gabo Zigamba mwenyewe ambaye ndiye muhusika mkuu wa Baraluko, Zulfa Msomali, Mary Mawigi, na wengine wengi, ikionesha maisha ya ndoa, familia, usaliti, changamoto za mahusiano, huku ikitunza na kuenzi mila na tamaduni za Kitanzania.

 

Wengi wamekua wakijiuliza wataipata wapi Baraluko na kwa gaharama ya kiasi gani basi tuwato shaka kwamba tamthiliya hii itapatikana bure kabisa kupitia YouTube channel ya Gabo Zigamba, kwa kila wiki pia vilevile na vipindi vingine vitaendelea kutolewa kila wiki kupitia channel yetu.

 

Kufuatia maelezo hayo ni hahiri kabisa tamthilia yetu ipo tayari kwaajili ya watazamaji wetu na kuanzia tarehe 14 mwezi Mei mwaka huu 2025 sehemu ya kwanza ya Baraluko itakua hewani kwa mara ya kwanza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet