pmbet

Garnacho alia kupewa dakika 20 fainali ya Europa League

Sisti Herman

May 22, 2025
Share :

Mustakabali wa winga wa kimataifa wa Argentina Alejandro Garnacho ndani ya kikosi cha mashetani wekundu Manchester United ni wa kutiliwa shaka baada ya kauli zake alizozitoa punde baada ya fainali ya Europa League jana usiku akionesha kukerwa na dakika chache alizopewa kukitumikia kikosi hicho kwenye mchezo huo muhimu wa fainali.

 



Garnacho aliwaambia waandishi wa Habari kuwa klabu yake imekuwa na msimu wa ‘hovyo’ mpaka sasa kwenye Ligi lakini yeye amepambana kwenye kila mechi aliyocheza na kuiwezesha United kufika fainali lakini ameshangazwa na kitendo cha kocha Amorim kumpa dakika 20 pekee kwenye mchezo wa fainali

"Ni ngumu kwetu sote. Msimu huu umekuwa wa ‘hovyo sana’. Tumepoteza fainali ya Europa League na hatujamfunga yeyote kwenye ligi kuu, kusema ukweli ni mbaya sana. Hadi kuifikia fainali, nilicheza kila raundi nikiisaidia timu, Halafu fainali inafika nacheza dakika 20 pekee? Kwakweli sijui na hili naona lina athari mbaya” alisema

Alipoulizwa ikiwa anataka kuondoka klabuni hapo kwakuwa ni wazi hajihisi kuthaminiwa Garnacho amesema kwa sasa anatamani Kwenda mapumziko ya majira ya joto kwanza akatafakari fainali hiyo, hali ya klabu na msimu kwa ujumla kisha ataamua

Awali kocha wa kikosi hicho Ruben Amorim akijibu swali kuhusu maamuzi yake ya kumuanzisha Mason Mount na kumuweka Bench Garnacho alisema lilikuwa ni kosa kubwa kufanya hivyo lakini ndio mpira ulivyo na kila mchezo una ‘approach’ yake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet