Guinea waangukia pua rufaa ya kudai alama 3 dhidi ya Taifa Stars.
Joyce Shedrack
June 16, 2025
Share :
Kamati ya rufani ya CAF imetupilia mbali rufaa ya Guinea dhidi ya Tanzania ya kuhitaji alama 3 dhidi ya Tanzania kwa madai kuwa beki wa kati wa Tanzania Ibrahimu Ame alivaa jezi yenye namba tofauti na ile iyoandikwa kwenye orodha rasmi ya wachezaji.
Guinea ilikata rufani kupinga uamuzi wa awali wa Kamati ya Nidhamu ya CAF kutupa malalamiko yao dhidi ya Tanzania.
Timu hiyo ya Taifa imeshindwa kufuzu michuano ya AFCON 2025 baada ya kumaliza nafasi ya 3 kwenye kundi H nyuma ya Tanzania na DRC ambao wamefuzu kushiriki michuano hiyo itakayofanyika nchini Morocco.
Novemba 19,2024 Guinea ilipoteza mchezo dhidi ya Taifa Stars kwa goli 1-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kusema kitendo cha Ibrahim Ame kuvaa jezi yenye namba tofauti iliwaathiri kisaikolojia na kuwafanya wapoteze mchezo huo.
Kamati ya Rufani imekubaliana na uamuzi wa awali wa Kamati ya Nidhamu ya CAF kuwa madai hayo hayana mashiko.