Harmonize akataa ushauri kwenye penzi lake na Kajala.
Joyce Shedrack
January 23, 2026
Share :
Baada ya kusambaa uvumi wa kuvunjika kwa penzi la staa wa bongofleva Harmonize na Kajala, Harmonize amejitokeza hadharani na kuweka wazi kuwa hawajaachana na watu wapunguze ushauri kwenye mahusiano yao.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram mwanamuziki huyo anasema ushauri ni mwingi hivyo unawachanganya yeye na mke wake.
"Habari za asubuhi, Bila Shaka mnaendelea vizuri? Naomba kuchukua muda kidogo, kama unajali kuhusu mimi, naongea kutoka moyoni."
"Muda ninaporudi kwa mke wangu, nafurahia kuona watu wakitufurahia na kusema tunapendeza kuwa pamoja, tunavyopendana licha ya kupitia mengi. Nafarijika kuwa couple inayopendwa, nawaahidi kwamba ninataka kufanya naye maisha."
"Tafadhali, msitushauri, ushauri ni mwingi sana na mnamchanganya. Tuliyopitia hatuhitaji kushauriwa. Hatuna haja ya kuingiliwa na posts zenu."





