pmbet

Harry Kane kutwaa kombe lake la kwanza Beyern wakitangaza ubingwa leo.

Joyce Shedrack

May 3, 2025
Share :

Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na Timu ya Taifa ya Uingereza Harry Kane huwenda siku ya leo ikawa ni siku ya kihistoria kwenye maisha yake ya soka endapo klabu yake itapata ushindi dhidi ya RB Leipzig na kutangazwa rasmi mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.

England's Harry Kane into top 20 men's international scorers with Latvia  goal - PA Media

Bayern Munich ambao ni vinara wa ligi hiyo wanaihitaji alama tatu siku ya leo wakiwa ugenini dhidi ya RB Leipzig ili kufikisha alama 78 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote katika michezo iliyosalia ili kukamilisha msimu. 

 

Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa na mafanikio makubwa akifanikiwa kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa ligi kuu Uingereza akiwa na Tottenham Hostpur na mwaka 2018 aliibuka mshambuliaji bora wa Kombe la Dunia huku msimu uliopita pia akiondoka na kiatu cha ufungaji bora wa ligi kuu ya Ujerumani licha ya timu yake kutokuwa Mabingwa wa Nchi hiyo hajawahi kubeba kombe lolote mpaka sasa.

Kane anatarajia kupata medali yake ya kwanza ya dhahabu ikiwa ni msimu wa pili ndani ya Bundesliga akiwa na umri wa miaka 31.

 

Msimu huu mpaka sasa Kane amefunga magoli 24 na kutoa pasi 7 za magoli katika michezo 29 aliyocheza huku akiongoza mbio za ufungaji bora wa Bundesliga na siku ya leo atakuwa nje ya uwanja akiitumikia adhabu ya kadi za njano.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet