Hawa hapa wabakaji hatari kuwahi kutokea duniani
Eric Buyanza
April 14, 2025
Share :

Katika historia ya uhalifu wa ngono, kuna wahalifu waliovuka viwango vya kawaida kwa kuwa na idadi kubwa ya waathirika ama watu waliowabaka. 
Ingawa wapo wengine kesi zikiendelea, lakini hawa ni baadhi ya wabakaji waliofanya uhalifu wa kutisha zaidi duniani na kuhukumiwa kifungo. 
1. REYNHARD SINAGA (UINGEREZA)
Huyu ni mbakaji mwenye rekodi mbaya zaidi katika historia ya Uingereza. Yeye hakuwa anabaka wanawake, bali aliwalenga wanaume. Na alitumia njia ya kuwapa dawa za kupoteza fahamu na kutumia mwanya huo kuwaingilia.
Sinaga alifungwa maisha mwaka 2020 baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya na kuwabaka wanaume 48 katika nyumba yake ya kifahari mjini Manchester.
Polisi wanaamini kuwa mwanafunzi huyo alihusika kuwalenga zaidi ya wanaume 200.
2. JOÃO TEIXEIRA DE FARIA "JOHN OF GOD" (BRAZIL)
Huyu alifanya ubakaji kwa mamia ya wanawake. Baada ya miaka mingi ya shutuma, zaidi ya wanawake 600 walijitokeza kumshutumu kwa unyanyasaji wa kingono. 
3. BILLY JOE GODFREY (MAREKANI)
Mtu huyu alikutwa na hatia na alikiri kufanya mauaji ya watoto wa kiume 221, na ubakaji wa watoto wengine zaidi ya 200.
4. LUIS GARAVITO (COLOMBIA)
Anajulikana kama "The Beast" kwa sababu ya unyama wake. Garavito alihukumiwa kwa kuwabaka, kuwatesa, na kuwaua zaidi ya watoto wa kiume 138, ingawa idadi halisi inakadiriwa kuwa zaidi ya 200. Watoto hao walikuwa na umri kati ya miaka 6 mpaka 16. 
5. RICHARD ALLEN MINSKY (MAREKANI)
Anajulikana kama "The Con Artist Rapist". Mbakaji aliyebaka wanawake kwa takriban miongo miwili katika majimbo kadhaa nchini Marekani. Alitajwa kubaka wanawake zaidi ya 100 kwa nyakati tofauti. 





