Hoteli refu zaidi duniani
Sisti Herman
May 13, 2025
Share :
Jengo refu la Ciel lilipo Dubai ambalo ni hoteli ya kisasa lipo tayari kufunguliwa mwaka 2025, na kuwa hoteli refu zaidi duniani ikiwa na urefu wa mita 365 (futi 1,198).
Hoteli hii ya ghorofa 82 itakuwa na vyumba na vyumba vya kulala zaidi ya 1,000, migahawa mitatu ya kipekee, na bwawa la juu zaidi la infinity huko Dubai.
Imebuniwa na NORR Group ya London na kuendelezwa na The First Group, Ciel tayari imeshinda tuzo nyingi za kimataifa za mali.