Huenda mfaransa Kolo Muani akaibukia Old Trafford
Eric Buyanza
January 11, 2025
Share :
Marcus Rashford akiuchungulia mlango wa kutokea, kumeilazimu Manchester United kuangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Randal Kolo Muani.
Hata hivyo mshambuliaji huyo wa kifaransa hajafanya vizuri tangu ajiunge na PSG, akiwa amefunga mabao 11 na kutoa asisti saba kwenye michezo 54.
Uhusiano kati ya Kolo Muani mwenye umri wa miaka 26 na kocha wake Luis Enrique, sio mzuri. Enrique amemuweka nje ya kikosi kwenye mechi mbili zilizopita za ligi.
Sky Sports (Ujerumani) inasisitiza kwamba United imedhamiria kufanya kila linalowezekana kumnasa mchezaji huyo msimu huu.
Hata hivyo, kunaonekana kutakuwa na mchuano mkali kwenye kuipata huduma ya mchezaji huyo kwani Chelsea, Aston Villa, Tottenham, Juventus, AC Milan, wanamfuatilia mchezaji huyo kwa ukaribu.