Ili Lamine Camara asimwage maua unamuhitaji Ngoma au Deborah
Eric Buyanza
May 23, 2025
Share :
Mkakati wa Kudili na Lamine Camara ilikuwa mzuri tu,tatizo ni utekelezaji wake..✍️
Jean Charles Ahoua Kupewa hili Jukumu Kimuundo ilikuwa sahihi Lakini Kiutekelzaji Kwa Sifa zake ni Kosa.
Kumfanya Lamine Camara asimwage Maua unamhitaji Labda Fabrice Luamba Ngoma au Deborah Fernandez Mavambo Kwenye #10
Kivyovyote itakavyokuwa ili HII TUNABEBA ikamilike wanahitaji Ku adjust sana na Kuongeza aggressiveness hasa Kuanzia Kwenye Mstari wa Juu ambao ulianza na Ateba na Jean Charles Ahoua Kwenye 4-4-2
Kumbuka Lamine Camara alikuwa anashuka Mpaka Kwenye Mstari wao wa Mwisho wenye Yusuph Dayo na Adil Tahif
Dhidi ya Ateba na Ahoua hapa tayari Berkane walikuwa na Faida ya mtu mmoja wa Ziada. Walipiga Pasi nyingi sana Bila Kupingwa nyuma ya Chamoe na Hamza.
Fadlu Davids anapaswa Kwanza Kuibadilisha hii hali kwa Kubadilisha watu au wenyewe watu Kubadlika.
Simba sports atahitaji Performance ambayo hatujawahi Kuiona Msimu huu.
Sema Mpaka hii mechi ikiisha Wachawi ndo watakuwa hoi zaidi Kuliko hata wachezaji.
Wachawi 👋🤣 HI
Ameandika mchambuzi wa michezo kutoka EFM @mzeewajambia