pmbet

Iran yasema imeidungua 'Droni' aina ya MQ 9 ya Marekani

Eric Buyanza

July 16, 2026
Share :

Iran imesema imeidungua na kuharibu ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ 9, ambayo inadai ilikuwa ikiruka juu ya mji wa Andimeshk.

 

Kwa mujibu wa Jeshi la Iran, ndege hiyo ilidunguliwa kwa kutumia mfumo wa kisasa wa ulinzi wa anga.

 

Shirika la habari la Tasnim, liliripoti kuwa operesheni hiyo ilifanikiwa, lakini halikutoa ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.

 

Hadi sasa, Marekani wala Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) hawajathibitisha rasmi madai ya Iran kwamba ndege hiyo ya MQ 9 ilidunguliwa.

 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet