Irene Uwoya amvaa mwanamke aliyehoji wokovu wake.
Joyce Shedrack
August 26, 2024
Share :
Msanii wa bongomovie Irene Uwoya amemvaa mwanamke ambaye video yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii akionekana kuhoji kuhusu wokuvu wa msanii huyo ambaye alitangaza kumrudia Mungu miezi michache iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo alichapisha ujumbe akimjibu mama huyo kabla ya muda mfupi kuufuta ujumbe huo.
"Biblia imeandika watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, naomba kumuuliza huyu mama lini amewahi kuja kanisani kwangu? nani alimwambia nina kanisa? nani alimwambia mimi mchungaji?
"Kuna watu wanapenda sana kukwaza watu yaani mtu uongee ujikute umemtukana mtu iwe shida nilisema sitaongea ila acha niseme.
Naomba anayemjua huyu mama amwambie akaangalie YouTube yangu nimeongea kila kitu.
"Pia mwambieni Mungu ndiyo ameniita sijajiita, pia ajue kwamba hii njia nilipo siyo rahisi naomba asiniongezee ugumu nikamkosea Mungu pia mimi ni Mkatoliki tangu nazaliwa ila namtumikia Mungu jinsi alivyoniagiza nafuata maelekezo ya Mungu na siyo binadamu aache kuropoka vitu hajui kama mwehu sababu anaonekana amechanganyikiwa," ameandika Irine.
"Naomba sana achunge mdomo wake maana sisi wengine tukilia kwa Mungu ni tatizo na mimi namhitaji bado aje ashuhudie ukuu wa Mungu ndani yangu," amesema Irene.





