pmbet

Ishowspeed wa Ethiopia apondwa kutojua Kingereza

Sisti Herman

January 15, 2026
Share :

 

Kijana wa Ethiopia anayefanana na staa wa mitandao ya kijamii IShowSpeed ameendelea kukumbwa na wimbi la ukosoaji kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wao wakimlinganisha na IShowSpeed wa Zimbabwe ambaye anaonekana kupendwa zaidi na mashabiki.

Kwa mujibu wa maoni ya wengi, IShowSpeed wa Zimbabwe ameweza kuvutia kwa kiwango kikubwa kutokana na uchangamfu wake, kujiamini na zaidi uwezo mzuri wa kuzungumza Kiingereza, jambo linalomfanya aonekane yupo tayari zaidi kubeba brand hiyo kimataifa.

Wengi wanasema tofauti kubwa kati yao ni mawasiliano, ambapo kwa upande wa Ethiopia, kijana huyo bado anaonekana kuwa na changamoto katika lugha ya Kiingereza, hali inayowafanya baadhi ya watu kuhoji kama yupo tayari kwa fursa kubwa anazoanza kukutana nazo.

Hata hivyo, wapo wanaoendelea kumtetea wakisisitiza kuwa kila mtu ana safari yake, na kwamba umaarufu haupimwi kwa lugha pekee. Wanasema badala ya kulinganisha na kukosoa, ni vyema kumpa muda na kumsaidia kujifunza ili aweze kufikia kiwango kizuri kama ilivyo kwa mwenzake wa Zimbabwe.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet