Jay Melody atikisa Boomplay afikisha streams milioni 300.
Joyce Shedrack
August 30, 2024
Share :
Mwanamuziki wa Bongo Fleva Jay Melody amefikisha zaidi ya streams milioni 300 kupitia mtandao wa kuuzia muziki wa Boom Play Music akiwa na zaidi ya nyimbo 40 kwenye akaunti yake ikiwa ni mwaka mmoja tangu alipofikisha streams milioni 200 mwaka 2024.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mtandao wa Boom Play wamethibitisha hilo baada ya kuchapisha taarifa inayoeleza kuwa Jay Melody amefikisha streams milioni 300 mwaka huu.
Kupitia mtandao huo wimbo unaoongoza kwa streams katika akaunti ya Jay ni ‘Nakupenda’ wenye zaidi ya streams milioni 82, huku mpaka kufikia sasa unazaidi ya wasikilizaji milioni 33 kupitia mtandao wa YouTube.
Ikumbukwe kuwa siku ya jana msanii huyo ameingia katika kinyanganyiro cha kuwania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa mwaka kupitia wimbo 'Nitasema' tuzo zilizopo chini ya waaandaji wa Tuzo za muziki Tanzania TMA.





