pmbet

Jay Melody kutikisa na albamu yake mpya aliyomshirikisha Alikiba.

Joyce Shedrack

May 7, 2025
Share :

Staa wa Bongo Fleva Jay Melody ametangaza kuachia albamu yake ya pili itayokwenda kwa jina la 'Addiction' siku ya Ijuma tarehe 9 Mei,2025.

Jay Melody amethibitisha taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiweka wazi kwa mashabiki wake kuwa albamu hiyo mpya ipo tayari.

"Mpendwa muziki, asante kwa kusafisha kichwa changu kila mara, kuniponya moyo wangu, na kuinua imani yangu. muziki ni uraibu kwangu," ameandika Jay Melody

 

Albamu hiyo itakayokuwa na ngoma 12 huku ngoma tatu akiwa amewashirikisha wasanii wakubwa akiwemo Alikiba, Mwana FA ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Juma Jux.

Ikumbukwe albamu ya kwanza ya Jay Melody aliiachia albamu April 26 mwaka jana iliyofahamika kama Therapy.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet