pmbet

Jeshi la Polisi laweka wazi sababu za kukamatwa kwa Amani Golugwa.

Joyce Shedrack

May 13, 2025
Share :

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetoa taarifa kuhusu kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Naibu Katibu Mkuu Chadema Golugwa Adaiwa Kukamatwa JNIA, Dar – Global  Publishers
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, imeeleza kuwa Golugwa alikamatwa Mei 13, 2025 majira ya saa 6:45 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa kwenye maandalizi ya kwenda Brussels, Ubelgiji.

 

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa kukamatwa kwa kiongozi huyo wa juu wa chama cha upinzani kulitokana na “taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi Nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa Nchini.”

Kwa sasa, uchunguzi wa kina unaendelea ukishirikisha Vyombo vingine vya Usalama, huku Polisi wakiahidi kutoa taarifa zaidi kadri hatua zitakavyopigwa.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizi za kisheria zinazomhusu mtajwa,” inasema taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet