JKT yaipeleka Simba Tanga
Sisti Herman
May 1, 2025
Share :
Klabu ya JKT Tanzania imepanga kucheza mechi yake ya Ligi Kuu dhidi ya Simba, Mei 5, 2025 katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga badala ya Uwanja wake wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam.
Uamuzi wa JKT Tanzania kupeleka mechi hiyo katika Uwanja wa Mkwakwani umefikiwa baada ya kufungwa kwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati wa mwisho kuupa utayari wa kutumika kwa ajili ya mazoezi ya timu zitakazoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika wa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN) 2025 mwezi Agosti mwaka huu.