pmbet

Jose Mujica, aliyekuwa Rais maskini zaidi duniani afariki dunia

Eric Buyanza

May 14, 2025
Share :

Rais wa zamani wa Uruguay José Mujica, anayejulikana kama "Pepe", amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.

Mpiganaji huyo wa zamani ambaye alitawala Uruguay kuanzia 2010 hadi 2015 alijulikana kama "rais maskini zaidi" kwa sababu ya kuishi maisha yake ya kawaida.
Rais wa sasa Yamandu Orsi alitangaza kifo cha mtangulizi wake kwenye jukwaa la X kwa kuandika: 

"Asante kwa kila kitu ulichotupa na kwa upendo wako mkubwa kwa watu wako."
Chanzo cha kifo cha mwanasiasa huyo hakijajulikana lakini alikuwa akiugua saratani.

Ni kawaida kukuta maisha wanayoishi Wanasiasa ni tofauti na wapiga kura wao lakini sio hivyo kwa aliyekuwa Rais wa Uruguay, Jose Mujica ambae anaishi kwenye maeneo ya mashambani na anatoa sehemu kubwa ya kipato chake kusaidia watu masikini.

Kutokana na hulka ya Viongozi na watu wengi kutaka kutukuzwa na kupewa kipaumbele hasa katika kupata huduma za kijamii, Mujica alikuwa akikaa kwenye foleni kutaka kumuona daktari katika hospitali ya umma.

Mpaka umauti unamkuta alikuwa akilindwa na Polisi wawili na mbwa na aliikataa kuishi kwenye nyumba ya Serikali aliyopewa na badala yake kaenda kuishi kwenye nyumba ya mke wake huko mashambani ambako kuna mazingira ya kimasikini sana ikiwemo barabara mbovu. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet