Jumapili tuna jambo letu zito la kitaifa - Naibu Spika
Eric Buyanza
May 24, 2025
Share :
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amewakumbusha wabunge wa bunge hilo kuwa Jumapili hii kuna jambo muhimu la kitaifa.
Akizungumza wakati akihitimisha shuguli za bunge, Zungu amesema historia inakwenda kuandikwa siku ya Jumapili.
Ifahamike kwamba Jumapili kikosi cha Simba kitacheza fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane ya Morocco.
Mchezo wa kwanza Simba ilipoteza 2-0, lakini wanaamini watapindua meza na kutwaa ubingwa siku ya Jumapili visiwani Zanzibar.