pmbet

Justine Bieber akiri jambo la maana alilolifanya ni kumuoa Hailey.

Joyce Shedrack

May 21, 2025
Share :

Staa wa muziki kutoka Canada Justine Bieber ameonekana kufurahishwa na uwepo wa mke wake kwenye maisha yake huku akikiri kuwa moja ya jambo la maana alilowahi kulifanya katika maisha yake ni maamuzi ya kumuoa mke wake Hailey Bieber.

 

Msanii huyo ambae hivi karibuni amekuwa akiripotiwa kupitia changamoto ya afya ya akili na ukosoaji mwingi kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kubadalika kwa mtindo wake wa maisha amesema amefanya mambo mengi ya kipumbavu lakini jambo la maana ni kumchagua Hailey kuwa mke wake.

Justin Bieber slammed for back-handed Instagram compliment over wife Hailey  landing Vogue cover | The Independent
“Nimefanya mambo mengi ya kipumbavu maishani mwangu, lakini jambo la busara zaidi ambalo nimewahi kufanya ni kumuoa Hailey,”amesema Bieber.

 

Bieber ameweka wazi kuwa licha ya magumu anayopitia lakini mke wake hajamkatia tamaa na amekuwa akipigana sana kujaribu kuwafanya watu wamuelewe.

"Amepigana sana kujaribu kuwafanya watu wanielewe, au kujua mimi ni nani, au kuniona kwa ajili yangu lakini watu hawataki. Amesema Bieber.

 

Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2018 na mpaka sasa wamejaliwa mtoto mmoja wa kiume  anayeitwa Jack Blues Bieber.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet