pmbet

Kambi ya Jeshi yavamiwa nchini Mali, wanajeshi zaidi 30 wauawa

Eric Buyanza

June 3, 2025
Share :

Mashambulizi mawili yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi la Mali katika mji wa Timbuktu na katikati mwa nchi yamesababisha vifo vya makumi ya wanajeshi pamoja na washambuliaji kadhaa.

Taarifa ya jeshi imesema wanajeshi wasiopungua 30 wamepoteza maisha kufuatia shambulio katika kambi ya kijeshi ya Boulkessi katikati mwa Mali. Taarifa hiyo imeongeza kwamba washukiwa 31 wa ugaidi tayari wamekamatwa.

Chanzo kingine ambacho kilizungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina kimesema wanajeshi 60 wamepoteza maisha.

Mali iliyo chini ya utawala wa kijeshi imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi kutoka kwa makundi yenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda na kundi linalojiita dola la kiislam la IS pamoja na magenge ya uhalifu mara kwa mara.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet