Karia akabidhi ofisi kwa Rais mpya wa CECAFA
Sisti Herman
May 4, 2025
Share :
Rais wa Shirikisho la soka Tanzania Wallace Karia., aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo ukanda wa CECAFA, amekabidhi rasmi ofisi kwa Augustino Maduot Parek ambaye amechaguliwa kuwa Rais mpya wa CECAFA.
Parek ambaye ni Rais wa Shirikisho la soka la Sudan Kusini anamrithi Karia ambaye ameteuliwa kuwa Mjumbe mpya wa Kamati ya Utendaji ya CAF (CAF EX-COM).
Katika utawala wa Karia ambaye ni Rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania alifanikiwa kukuza soka katika ukanda wa CECAFA na kufufua mashindano yaliyokuwa yamekufa.
Mbali ya hayo, Karia amefanikiwa kulikuza soka la Tanzania ambalo limekuwa kivutio kwa Afrika na wachezaji mbali mbali wanaovutiwa kusakata soka.