Karia aongoza ujumbe wa Tanzania FIFA
Sisti Herman
April 30, 2025
Share :
Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye warsha ya Shirikisho la soka Duniani (FIFA) inayohusisha nchi Wanachama wa UEFA na CAF inayofanyika Vienna, Austria.
Kwa mujibu wa taarifa ya mtandao wa CAF, nchi zinazohudhuria kwenye warsha hiyo ya kuimarisha maendeleo ya soka duniani ni Finland, Moldova, Wales, Austria, Georgia kutoka UEFA, Morocco, Senegal, Tanzania na Cameroon.