Kauli mbiu ya Simba Nusu Fainali ni HATUISHII HAPA.
Joyce Shedrack
April 15, 2025
Share :
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amezindua hamasa kuelekea mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini huku akitangaza kauli mbiu ya mchezo huo kuwa ni ‘HATUISHII HAPA’.
“Kaulimbiu ya kuingia nusu ilikuwa HII TUNAVUKA na tukafanikiwa lakini kuelekea fainali tunakuja na HATUISHII HAPA. Tunatoka hatua hii tunakwenda fainali. Malengo yetu ni kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.”
“Kila mtu ni siri yake anajua alifanya nini Simba kufika nusu fainali. Wachezaji wanajua walipambana vipi Simba inafika nusu fainali, viongozi wanajua walipambana vipi, benchi la ufundi wanajua walitumia mikakati gani. Rai yangu kila alichofanya mtu kuipeleka nusu fainali kwenye mechi hii ya kuipeleka fainali basi azidishe mara tatu yake.”
“Inawezekana sana Simba kucheza fainali sababu ubora huo tunao na kila kitu kimekaa vizuri. Na bahati nzuri fainali tutaanzia ugenini na kumalizia nyumbani. Tushindwe nini? Haleluya.”- Semaji Ahmed Ally akiongea na wanahabari visiwani Zanzibar.