pmbet

Kenya, Uganda na Tanzania kuanzisha VISA ya pamoja CHAN

Sisti Herman

May 11, 2025
Share :

Kenya, Uganda na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatazamiwa kujadiliana kuhusu uteuzi wa mwisho na utayarifu wa maeneo ya kuandaa Sherehe za ufunguzi na kufunga, pamoja na mchujo wa 1, 2 na wa tatu wa michuano ijayo ya ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), yaliyopangwa kufanyika Agosti 2025.

 



Wakati wa Mkutano wa Mawaziri kwa njia ya mtandao ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CAF Veron Mosengo-Omba, Waziri wa Masuala ya Vijana wa Kenya, Uchumi wa Ubunifu na Michezo, Mhe. Salim Mvurya, alisisitiza kujiandaa kwa nchi kuandaa Sherehe na Mechi.

Pia yalifanyika mapendekezo yaliungwa mkono na Mhe. Peter Ogwang, Waziri wa Michezo wa Uganda, na Mhe. Hamisi Mwinjuma, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Waziri wa Kenya alisisitiza utayari wa pamoja na dhamira ya nchi zao katika kuandaa CHAN 2025 yenye umoja.

Mataifa hayo matatu pia yalijadili hatua za kuwezesha namna ya kuvuka mipaka ambapo miongoni mwa mapendekezo ni kuanzishwa kwa PAMOJA VISA au pasi maalumu ya kuingia mara nyingi ili kurahisisha kuvuka mipakani hasa kwa wachezaji na mashabiki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet