pmbet

Keown ampigia chapuo Klopp ili amrithi Amorim Man U

Eric Buyanza

June 3, 2025
Share :

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Martin Keown, amewataka Manchester United kuachana na Ruben Amorim na kumpa kibarua hicho kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp.

 

Kwa mujibu wa Keown, Klopp ana uzoefu zaidi ya Amorim na atafanya kazi iliyotukuka kuliko hichi anachokifanya Amorim.

 

"Bado nina wasiwasi huenda Ruben Amorim sio kocha sahihi kwa Manchester United," Keown alisema kwenye mahojiano na talkSPORT.


"Angalia tu idadi ya michezo ambayo wamepoteza chini ya Amorim”

"Naamini Klopp anaweza kufanya kazi nzuri sana Manchester United na wanahitaji mtu mwenye uzoefu zaidi kuliko Amorim."

 

Klopp kwa sasa hana timu baada ya kuondoka Liverpool kabla ya kuanza kwa msimu wa 2024/25.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet