Kesi imeshakuwa ngumu...!Yanga yasisitiza kuidai TFF fedha za ubingwa.
Joyce Shedrack
June 10, 2025
Share :
Klabu ya @yangasc imetoa taarifa jioni ya leo ikijibu taarifa ya TFF iliyotolewa msaa machache yaliyopita huku wakisisitiza kuwa wanahitaji kulipwa fedha zao za ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB kwa msimu uliopita ili wacheze mchezo wa fainali juni 28 mwaka huu.
Yanga imesema hakuna uthibitisho wowote wa kimaandishi kuonyesha kama TFF wamewahi kulipa fedha hizo za Ubingwa kwa Klabu ya Yanga na kusisitiza kuwa ni aibu na fedheha na kumtia dosari mdhamini kuendesha mashindano bila kumlipa Bingwa kwa misimu mitatu mfululizo.
“Tunaelekeza, dawa ya deni ni kulipa kwa wakati ikiwa ni haki ya mshindi na inampa heshima mdhamini wa mashindano. leleweke, ada za malipo ya wachezaji wa kiger kigeni walizozisema kwenye taarifa yao hulipwa mwanzo wa msimu mpya na hela hizi za Ubingwa hutolewa Mwisho wa msimu.”
“Klabu ya Young Africans haijawahi kupokea taarifa yoyote rasmi kutoka TFF kuhusu Klabu yetu kuwa na deni kwao. Uongozi wa Klabu ya Young Africans unaendelea kusisitiza kulipwa pesa yake ya Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB, kwa msimu wa 2023/24 ili tuweze kucheza mchezo wa Fainali siku ya tarehe 28 Juni, 2025.” -imesema Yanga Sc