Kesi ya Mwijaku na Masoud Kipanya kusikilizwa Septemba
Joyce Shedrack
August 8, 2024
Share :
Mtangazaji Masoud Kipanya amemfungulia kesi ya madai ya udhalilishaji kupitia mitandao, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku ambapo ameiomba Mahakama Kuu imwamuru Mwijaku amlipe fidia ya Tsh. Bilioni 5.5 na gharama nyingine za Kesi.
Mwijaku ametuhumiwa kumkashifu, kumshushia hadhi na heshima na kuandika taarifa za uongo Mitandaoni, jambo ambalo Masoud amedai limemuathiri Kiajira, Kibiashara, Kimahusiano na Kisaikolojia.
Juni 2024 kupitia Mitandao ya Kijamii Mwijaku anadaiwa alichapisha taarifa akimtaka Masoud Kipanya aache kumfuatilia, pia alidai Masoud anafanya biashara haramu na amekuwa akihongwa kuwasema Viongozi na Serikali.