pmbet

Kesi ya Ubakaji yasepa na Bilioni 51 za Jay Z.

Joyce Shedrack

March 4, 2025
Share :

Rapa maarufu wa Marekani Jay-Z amefungua kesi ya kudhalilisha jina lake dhidi ya mwanamke Jane Doe aliyemfungulia Mashtaka kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia, pamoja na wakili wake Tony Buzbee ambao waliifuta kesi hiyo februari 14 mwaka huu.

Jay-Z: Life, Legacy and Influence

Jay-Z amefungua kesi hiyo akidai kuwa tuhuma hizo za uwongo zimeharibu jina lake na kumgharimu kampuni yake ya Roc Nation kupoteza zaidi ya dola milioni 20 sawa na Tsh Bilioni 51.8.

Ikumbukwe,mwezi Desemba mwaka jana Jane Doe alifungua kesi dhidi ya Jay Z akidai alidungwa dawa za kulevya na kubakwa baada ya tafrija ya Tuzo za Muziki za MTV mwaka 2000, akiwa na umri wa miaka 13.

 

Mwanamke huyo amefichua kuwa aliamua kufuta kesi yake kwa sababu alimwogopa Jay Z na wafuasi wake akiweka wazi kuwa na hofu ya kutengwa hadharani na kushambuliwa hadharani na wafuasi wa rapa huyo.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet