Kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu yapigwa kalenda kwa mara nyingine.
Joyce Shedrack
May 6, 2025
Share :
Shauri la kesi ya Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu leo tarehe 06-05-2025 dhidi ya Jamhuri limetajwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Franko Kiswaga kwenye MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Kesi hiyo imeshindikana kusikilizwa tena kutokana na upande wa Mashtaka yaani Jamhuri kutokukamilisha upelelezi wa kesi hiyo uhaini dhidi ya Lissu, na kesi imeahirishwa hadi Mei 19-2025.
Hata hivyo mtuhumiwa Tundu Lissu hakutokea kwenye Mahakama ya mtandao, kutokana na kugomea kesi yake kusikilizwa kwa njia ya mtandao.
Upande wa utetezi yaani Mawakili wanao mtetea Lissu unadai hauridhishwi na jinsi upepelezi huo unavyosusua wakati kesi hiyo ni ya maneno ambayo Lissu aliyasema kweny mitandao.
Mahakama imeitaka Jamhuri kukamilisha ushahidi huo Mei 19 na kuleta Maelezo sahihi na kesi iweze kuanza.