pmbet

Kiongozi wa ACT akamatwa na Polisi Kimara

Sisti Herman

May 23, 2025
Share :

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita anadaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kutembelea mradi wa mwendokasi kuangalia kero wanazopitia wananchi.
 


Taarifa ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa ACT Wazalendo imetolewa na ofisa habari wa chama hicho, Abdallah Khamis leo Mei 23,2025.

"Alikuwa akifanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Stendi ya Mwendokasi Kimara Mwisho, lengo ikiwa ni kushuhudia namna ambavyo wananchi wanapitia changamoto katika usafiri huo wa umma,"amesema.

Abdalah amesema baadhi ya viongozi waliojitambulisha ni wafanyakazi wa mradi wa mwendo kasi, walimfanyia fujo kiongozi huyo wakitaka asipokee malalamiko ya wananchi katika kituo cha Kimara kutokana na madhila wanayoyapata katika usafiri huo.

"Kwa sasa Mchinjita anashukiliwa polisi, katika kituo cha polisi cha mwendokasi," amesema.

Hata hivyo alipotafutwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro kuthibitisha taarifa hizo na sababu ya kukamatwa kwa kiongozi huyo, simu yake ilita bila kupokelewa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet