pmbet

Klabu Leon yaondolewa kushiriki kombe la dunia ngazi ya klabu.

Joyce Shedrack

March 22, 2025
Share :

Shirikisho la soka Duniani (FIFA) limeiondoa klabu ya Leon ya Nchini Mexico kwenye michuano ya kombe la Dunia ngazi ya klabu kutokana na klabu hiyo kumilikiwa na mmiliki mmoja sawa na klabu ya Pachuca  inayoshiriki michuano hiyo.

14 bodyguards? The demands of James Rodriguez that Leon will fulfill | Marca
Klabu Leon na Pachuca zinamilikiwa na kampuni ya Grupo Pachuca hivyo Leon imekosa uhalali wa kushiriki michuano kutokana na kukiuka ibara ya 10 kifungu cha nne ya kanuni za Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA 2025 ambayo inabainisha kuwa vilabu viwili vilivyopo chini ya mmiliki mmoja haviwezi kushiriki michuano hiyo kwa pamoja.

FIFA imeamua kuiondoa kwenye mashindano hayo Klabu ya León ambayo ilikuwa imepangwa kundi D, sambamba na Flamengo, Chelsea na Espérance Sportive de Tunis.
 

Shirikisho hilo la Mpira wa Miguu Duniniani litatangaza timu nyingine kutoka ukanda wa CONCACAF itachukua nafasi ya klabu Leon huku Liga Deportiva Alajuelense ya Costa Rica ikitajwa kuwa miongoni mwa timu zitakazochukua nafasi hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet