pmbet

Kocha wa Orlando kurithi mikoba ya Hamdi Yanga

Sisti Herman

May 4, 2025
Share :

Klabu ya Yanga inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na kocha mkuu wa klabu ya Orlando Pirates Jose Riveiro kurithi mikoba ya kocha Miloud Hamdi anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.
 


Riveiro ambaye ametangaza rasmi kuondoka kwenye klabu ya Orlando mwishoni mwa msimu anaweza kurithi mikoba ya Hamdi.

Kocha Jose tangu ametua Orlando Pirates Julai 1, 2022, amefanikiwa kushinda mataji matatu ya Kombe la MTN na mawili ya Kombe la Nedbank huku msimu huu timu hiyo ikiishia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikipoteza mbele ya Pyramids.

Mbali na Yanga, pia kocha huyo ana ofa ya Saudi Arabia, huku pia akihusishwa na Al Ahly ambayo hivi karibuni iliachana na kocha Marcel Koller baada ya kushindwa kuifikisha timu hiyo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet