Kuwa na mahusiano na Wema kumenisogeza sana - Whozu
Eric Buyanza
June 13, 2025
Share :
Mwanamuziki Whozu amesema kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji Wema Sepetu kumemsaidia mambo mengi katika maisha yake.
“Kuwa na mahusiano na Wema Sepetu kumenisogeza sana, kwa sababu ni staa wa filamu kutoka kitambo sana na hata kwenye mambo ya urembo. Mimi nilikuwa najulikana, lakini nilivyokutana na Wema kuna vitu vingi vimeongezeka katika maisha yangu,” alisema Whozu.
MWANASPOTI