Lamine Yamal na Fermin Lopez kukiwasha dhidi Girona.
Joyce Shedrack
October 17, 2025
Share :
Kocha Mkuu wa Barcelona Hans Flick amethibitisha kuwa nyota wawili wa kikosi chake Lamine Yamal na Fermín López wamepona majeraha yao na watakuwepo katika mchezo wa ligi dhidi ya Girona.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo utakaopigwa siku ya kesho Flick amesema wachezaji hao wawili watakuwa tayari kucheza japo si kwa dakika zote 90.
Hata hivyo Hans Flick amesema katika mchezo huo watamkosa mshambuliaji Ferran Torres kutokana na maumivu ya misuli ya paja kwenye mguu wake wa kushoto.
Mshambuliaji huyo alipata tatizo hilo wakati wa mapumziko ya kimataifa, na madaktari wa klabu wameamua kumpumzisha ili kuepuka kuongezeka kwa jeraha.