pmbet

Lavalava kujiengua WCB Wasafi Baba Levo athibitisha.

Joyce Shedrack

May 8, 2025
Share :

Mtangazaji wa Wasafi Fm Baba Levo ameandika ujumbe unaoonekana kuthibitisha kuwa Lava Lava ameondoka rasmi kwenye lebo ya WCB Wasafi huku akimshukuru na kumtakia kila nla kheri kwenye safari yake ya mziki.

Lava Lava Ft Diamond Platnumz - Tuna Kikao (Official Music Video)

Baba Levo ameandika ujumbe ufuatao kwenye ukurasa wake wa Instagram “THANK YOU ..! 🙏Safari Njema Mdogo Wangu Una Kipaji Kikubwa Sana @iamlavalava Na Watanzania Watakuwa Mashahidi kwa namna ambavyo Mzee wangu LUKUGA alikipigania kipaji chako kibadilike kuwa pesa...”-Baba Levo.

Msanii huyo ambaye alijiunga na WCB Wasafi mwaka 2017 bado hajathibisha kuondoka ndani ya lebo hiyo licha ya kuwa mkataba wake unaelekea ukingoni bado hakuna taarifa rasmi kutoka WCB wenyewe juu ya kuondoka kwa msanii huyo huku yeye pia mwenyewe mpaka sasa bado hajabadilisha profile yake kwenye ukurasa wake wa instagram.

 

Lavalava akiwa chini ya lebo hiyo alitamba na ngoma kali zilizomtambulisha zaidi kwenye soko la sanaa hiyo kama 'Tuachane', ‘Habibi, ’Tajiri, ‘Nga’ring’ari’ na nyingine nyingi.

 

Ikiwa staa huyo ataachana na lebo hiyo ataungana na wasanii wengine ambao walijiengua kwenye lebo hiyo akiwemo Harmonize,Rich Mavoko,Mbosso na Rayvanny.



 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet