Luis Figo amkimbia mke, amuachia nyumba na kwenda kupanga
Eric Buyanza
April 26, 2025
Share :
Gwiji wa soka, Luis Figo ameripotiwa kuikimbia nyumba yake huku akimuacha mkewe Helene Svedin na kwenda kuishi kwenye nyumba ya kupanga.
Haya yanajiri baada ya mreno huyo kuhudhuria tuzo za Laureus nchini Uhispania mapema wiki hii, ambapo kwenye moja ya mahojiano alitaja mambo 'bora' maishani mwake akiwataja mabinti zake Daniela, Martina, na Stella, bila kumtaja mkewe.
Vyombo vya habari mbalimbali vimeripoti kuwa Figo na mkewe Svedin kwasasa wanaishi maisha ya 'kila mtu kivyake', hata hivyo hakuna taarifa rasmi za wawili hao kutengana.
Figo na Svedin wamekuwa pamoja tangu 1996, baada ya kukutana kwenye karamu ya chakula cha jioni katika mwaka wake wa kwanza huko Barcelona.
Wanandoa hao walichumbiana kwa miaka mitano kabla ya kufunga pingu za maisha, miaka miwili baada ya kuzaliwa kwa binti yao mkubwa, Daniela.
Figo amekuwa akihusishwa na mwanamitindo wa kihispania Claudia Bavel.