Lukuvi, Kabudi na Makonda wawasili Arusha
Sisti Herman
August 23, 2024
Share :
Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. William Vangimembe Lukuvi, Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda, kwenye picha ya pamoja walipowasili kwenye Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Ambapo pamoja na shughuli mbalimbali walizopangiwa kuzifanya Wilayani Karatu, Leo Ijumaa Agosti 23, 2024 wamekutana na Kamati ya Ulinzi na usalama mkoa wa Arusha kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Katika ziara hiyo ya Kikazi viongozi hao wameambatana na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Juma Haji.