Madrid na Arsenal walitaka kumsajili Messi.
Joyce Shedrack
September 11, 2024
Share :
Aliyekuwa wakala wa kwanza wa Lionel Messi,Horacio Gaggioli ameweka wazi kuwa Klabu ya Real Madrid na Arsenal ziliwahi kuhitaji huduma ya mchezaji huyo kwa nyakati tofauti ila Messi alikataa kuondoka Barcelona.
Gaggioli amefunguka hayo akiwa kwenye mahojiano huku akisema Madrid waliwahi kumuhitaji nguli huyo wa Barcelona akiwa na umri wa miaka kati ya miaka 16 na 17 lakini Messi alitaka kutengeneza historia na kupata mafanikio akiwa Barcelona.
“Real Madrid walivutiwa naye alipokuwa kijana akiwa na umri wa miaka 16-17, lakini Leo hakuwahi kutaka kuondoka Barca ni kweli Arsenal walionesha nia ya kuhitaji saini yake mapema sana lakini mchezaji hakutaka kuondoka Barca”amesema Gaggioli.
Messi alijiunga na timu ya vijana ya Barcelona mwaka 2001 kabla ya kuanza kuitumikia klabu hiyo kwenye kikosi cha Barcelona mwaka 2004 na kuanza kuvuna mafanikio makubwa na kikosi cha wakubwa cha timu hiyo na kuondoka klabuni hapo kama mchezaji nguli wa Barcelona.
Mshindi huyo wa Ballon d'o mara nane alilazimika kuondoka Barcelona mwaka 2021 kutokana na sheria ya kiuchumi iliyowekwa na Laliga na kutimkia PSG nchini Ufaransa kabla ya kujiunga na Timu yake ya sasa ya Inter Miami Nchini Marekani.