Madrid wanamtaka David Raya akawe mrithi wa Thibaut Courtois
Eric Buyanza
May 12, 2025
Share :
Mlinda mlango wa Washika Bunduki wa jiji la London, David Raya yuko kweye rada za Real Madrid wakimtazama kama mbadala wa Thibaut Courtois, ambaye amefikisha miaka 33 wikIendi hii.
Hata hivyo Madrid wanaamini dili la kumpata mlinda mlango huyo nambari moja wa Arsenal huenda likawa sio rahisi sana kulikamilisha kutokana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kuwa chini ya mkataba pale Emirates hadi Juni 2028.