Mafua chanzo cha Ronaldo kuikosa game na Al-Taawoun
Eric Buyanza
May 17, 2025
Share :
Kocha wa Al-Nassr, Stefano Pioli ameeleza ni kwa nini nahodha, Cristiano Ronaldo alikosa mechi ya timu yake ya dhidi ya Al-Taawoun siku ya jana Ijumaa.
Ronaldo hakuwepo wakati Al-Nassr ikitoa sare ya 1-1 dhidi ya Al-Taawoun.
Mabao kutoka kwa Otávio na R. Martínez yalihakikisha timu zote mbili zilipata pointi moja kwenye uwanja wa Al -Awwal Park.
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya mechi, Pioli alisema fowadi huyo wa Ureno alikosa mchezo huo kwasababu ya kusumbuliwa na mafua makali.
"Ronaldo hayupo kwa sababu anaugua mafua," Pioli alisema.
Al-Nassr kwa sasa wako katika nafasi ya 4 kwenye Ligi ya Saudia wakiwa na pointi 64 katika michezo 32.