Magori ahoji vigezo vya IFFHS ligi ya Tanzania kuwa ya 4 Afrika
Sisti Herman
January 24, 2025
Share :

Ikiwa ni siku moja tangu Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) litangaze @ligikuu ya Tanzania (NBC Premier League) kuwa Ligi ya nne (4) kwa ubora barani Afrika na ya 57 duniani kwa mwaka 2024, Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba Crescentius Magori amehoji uhalali wa viwango hivyo vya ubora kwasababu vigezo ya vinavyotumiwa na shirikisho hilo kutokuwa bayana.
"Ina mapokeo mazuri kwa kila Mtanzania, lakini intakubali viwango vya ubora vya IFFHS pale tu watakapoweka hadharani vigezo wanavyotumia, kama wanavyofanya FIFA na CAF kupanga viwango vyao" aliandika Magori kwenye chapisho la mtandao wa kijamii la mwandishi wa habari Micky Jr aliyeandika habari hiyo.
Kwa mujibu wa IFFHS, Ligi ya Tanzania imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya sita mwaka 2023 ikizipiku Ligi za Afrika Kusini na Tunisia ikiwa nyuma ya vinara Ligi kuu Misri, Morocco iliyopo nafasi ya pili na Algeria ambayo ipo nafasi ya tatu huku Tunisia ikikamilisha tano bora kwa Afrika.
1. Nile Premier League — Egypt
2. Botola Pro League — Morocco
3. Ligue 1 — Algeria
4. NBC Premier League — Tanzania
5. Ligue 1 Pro — Tunisia





