Mahakama yaamuru Tundu Lissu aletwe mahakamani Mei 19.
Joyce Shedrack
May 6, 2025
Share :
Shauri lililowekwa April 24 kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu isikilizwe kwa njia ya mtandao, limeondolewa hii leo na Hakimu Mfawidhi Muhini wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kiongozi huyo mkubwa wa upinzani atapandishwa Mahakamani hapo Mei 19.
Upande wa utetezi uliwasilisha hoja la kuweka pingamizi kwa madai haki ya msingi ya mteja wao inakuwa inakiukwa na anakosa haki ya kuonana na Mawakili wake.
Hakimu Muhini amesema kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai inatoa haki mtuhumiwa kusikilizwa akiwa ndani ya MAHAKAMA.
Hakimu Muhini amesema kwa mujibu Ibara ndogo ya 6(A) kifungu Cha 13 Cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki kwa mshitakiwa kuletwa Mahakamani na kesi isikilizwe mbele ya Umma.
Mmoja wa Mawakili wa Utetezi Peter Kibatala amewakaribisha Wananchi kujitokeza Mahakamani hapo na kusikiliza kesi hiyo kwa Amani na utulivu