pmbet

Mahakama yafuta kesi ya Ubakaji ya Mbappe

Sisti Herman

December 13, 2024
Share :

Mahakama nchini Sweden imetupilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabiki mshambuliaji wa Real Madrid na Ufaransa Kylian Mbappe baada ya mwendesha mashtaka nchini humo kusitisha uchunguzi wa kesi kwasababu ushahidi haujitoshelezi.

Uchunguzi huo ulifunguliwa bila kulitaja jina la Mbappe, kufuatia ripoti za vyombo vya habari kudokeza nyota huyo wa ufaransa ndiye mshukiwa kufuatia ziara yake Mjini Stockholm.

Kwa kurejelea Makala zilizochapishwa kwenye magazeti ya Aftonbladet ,Expressen na shirika la utangazaji la umma la SVT Oktoba mwaka huu zilimtaja Mbappe ndiye muhusika.

Mara baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, shirika la habari la AFP liliwatafuta wawakilishi wa Mbappe ambao walisema hawahafahamu malalamiko yaliyotolewa dhidi ya mchezaji huyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet