Makadinali 133 kuanza mchakato wa kumchagua Papa leo
Eric Buyanza
May 7, 2025
Share :
Baraza Maalumu la Siri likiwa na jumla ya makadinali 133 linakusanyika leo mjini Roma kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa kanisa katoliki duniani.
Makadinali hao watajifungia kwenye kanisa dogo la Sistine kwa muda usiojulikana hadi pale mmoja miongoni mwao atakapofanikiwa kupata theluthi mbili ya kura na kutawazwa rasmi kuwa kiongozi mkuu wa kanisa hilo lenye waumini wapatao Bilioni 1.4.
Waumini wa kanisa katoliki kote duniani watasubiri ishara ya kuchaguliwa kwa Papa mpya kupitia moshi utakaotoka kwenye chimni iliyofungwa juu ya kanisa la Sistine.
Moshi mweupe utakapofuka itakuwa ni ishara kuwa baraza hilo la makadinali limefanikiwa kumchagua kiongozi mpya wa kanisa.