Makalla awaita G-55 kujiunga na CCM
Sisti Herman
May 8, 2025
Share :
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewaita G55 waliotangaza kuondoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujiunga na chama tawala ili katika Uchaguzi Mkuu CCM kishinde kwa kishindo.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, ameyasema hayo leo Mei 7, 2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Mvomero, mkoani Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku saba.
Amesema amewasikia G55 wametoa kauli wamesema wamechoka kukaa CHADEMA kwa sababu hakitashiriki uchaguzi ujao.
Kutokana na kauli hiyo, Makalla amewaambia pamoja na kuondoka CHADEMA, CCM inawakaribisha na milango iko wazi waende kujiunga chama tawala.
Amesema vyama 18 vitashiriki uchaguzi, kasoro kimoja hivyo anawakaribisha wajiunge CCM ili kushinda kwa kishindo.
“Lengo la chama chochote cha siasa ni kushika dola, ninawatabiria baada ya Uchaguzi Mkuu CHADEMA itakuwa jukwaa la wanaharakati.
“Watakuja huku siku moja kuwadanganya hawataki kuingia katika uchaguzi wanataka mabadiliko, Rais wetu ni msikivu marekebisho makubwa yamefanyika lakini hawataki kuwaambia wananchi,” amesema.